UTI isiyoisha inasababishwa na nini na dawa zake ni zipi?

UTI huhitimishwa kuwa sugu yaani “recurrent” pale ambapo:
1) Imethibitishwa kwa vipimo sahihi kuwa umepata UTI tatu au zaidi ndani ya miezi 12 au
2) Umepata maambukizi mara mbili au zaidi ndani ya miezi sita.
Kawaida vimelea vile vile zilizosababisha maambukizo ya hapo awali ndio huwajibika kwa kurudia.
Ni nini husababisha UTI ya mara kwa mara au isiyopona?
Sababu za UTI ya mara kwa mara kwa wanawake waliokoma hedhi (menopause) hutofautiana na wanawake ambao bado wanapata hedhi
Kwa wanawake walio katika kipindi cha kabla ya kukoma hedhi, zifuatazo ni sababu ambazo zinachangia
kutokua na usafi sahihi wa uke ikiwepo aina ya nguo nk.
kujamiiana mara tatu au zaidi kwa wiki
matumizi ya dawa za uzazi wa mpango za kuuwa sperm (spermicides)
wenzi wapya au wengi wa ngono
Kuwa na UTI kabla ya umri wa miaka 15
Kwa wanawake waliokoma hedhi, hatari huongezeka hasa kutokana na matokeo ya viwango vya chini vya vichochezi hasa, estrojeni.
Kwa nini unapaswa kuwa makini kuhusu kutafuta huduma?
UTI ambayo haijatibiwa au inatibiwa na dawa mbadala bila kuwa na vipimo sahihi inaweza kusambaa hadi sehemu za juu za mfumo wa mkojo kama kibofu, figo au hata katika hali mbaya sana kufikia damu. Hii inaweza kusababisha maambukizi makali zaidi yaitwayo sepsis.
Kutumia tu dawa za antibiotic bila vipimo sahihi kutasababisha ukinzani wa dawa na kutapelekea dawa kutofanya kazi na hivyo kupelekea kutuliza dalili tu bila kutibu kiuhakika.

Dalili zake ni zipi?
UTI inayojirudia kwa kawaida huwa na dalili zifuatazo
maumivu makali wakati wa kukojoa (kama kuwaka moto)
kubanwa na mkojo mara kwa mara
kusitasita kwa mkojo
Nini kinaweza kukusaidia kuzuia UTI
Kukojoa baada ya kujamiiana
Kunywa maji mengi
Kuoga na maji tiririka na sio kwenye bathtab au beseni
Usipake, vinyunyuzi vyovyote au poda kwenye sehemu ya siri
Tawaza kwa kufuta mbele kuelekea nyuma
Tiba
Nadharia za matibabu ya UTI inayojirudia inategemea upimaji vimelea vya bakteria, vipimo vya kuotesha vimelea ili kujua ni kimelea kipi kitatibika na dawa ipi, nk.. Kwa kawaida ni mchanganyiko wa matibabu na elimu ya usafi wa uke.
Tiba ya kinga - kuzuia vizuia vimelea
Tiba endelevu ya antibiotics kutegemeana na utofauti wa viashiria
Antibiotic dose za papo hapo na muda mfupi
Tiba ya jumla - kuangalia shida nyingine za kimaumbile na kuhakikisha hamna mchanganyiko wa magonjwa mengine kama STI nk..
Hitimisho
Kama umeshatumia dawa au suluhisho nyingine bila mafanikio, pata ushauri wa daktari aliyebobea kwa kupiga au whatsapp 0763 1000 93